miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
MPANDA
Katibu wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi itikadi na uenezi Shaka Hamdu shaka ameiagiza wizara ya ujenzi wa bandari ya Karema kwenda sambamba na ujenzi wa barabara ili kukamilisha ilani ya uchaguzi wa mwaka 2020/2025.
Ameyasema hayo wakati akikagua miradi mkoani katavi na kusema kuwa moja ya jambo walilo liahidi katika kukamilisha ilani ya uchaguzi wa CCM ni ujenzi wa bandari ya Karema ili kufungua uchumi wa wananchi .
Kwa upande wake mhandisi mkazi katika bandari ya Kalema Eng. Elisante Urassa amebainisha ujenzi wa bandari hiyo na kusema kuwa hadi sasa bandari imefikia ujenzi kwa asilimia 66. Mradi wa ujenzi wa bandari ya Karema wilaya ya Tanganyika mkoani katavi umeanza kujengwa mnamo mwaka 2019 na unatarajiwa kukamilika mnamo march, 2022.