miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
TANGANYIKA
Wananchi wakijiji cha Vikonge kata ya Tongwe wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi wamepongeza jitihada zinazo fanywa na serikali katika kutekeleza mradi wa maji kijijini hapo.
Wakizungumza na mpanda redio fm wananchi hao wamesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutawapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji.
.
Kwa upande wake mwenyekiti wakijiji hicho Joseph Sungulu amesema serikali ilitoa kiasi cha shilingi milioni mia sita ili kukamilisha mradi huo na tayari mabomba ya maji yamesambazwa na mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi wa kumi mwaka huu.
.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amewataka wananchi kuwa waangalifu pindi mradi huo utakapokamilika na kutunza miundombinu hiyo ya maji.