miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
MPANDA
Watumiaji wa vyombo vya moto Halmashuri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi walalamikia ubovu wa miundombinu ya Barabara na kutaka marekebisho yafanyike na mamlaka husika.
Wakizungumza na Mpanda Redio FM wamesema kuwa hali ya Barabara sio ya kuridhisha kwani Barabara nyingi zimeharibika na kuchimbika mashimo ambayo imekuwa sababu ya kupelekea ajali, kuharibika kwa vyombo vya moto na kuiomba serikali kutatua changamoto hiyo.
Hoza Joseph ni Meneja wa Mamlaka wa Barabara za mjini na vijijini TARURA wilaya ya Mpanda wamesema kuwa tayari wameshaomba fedha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kuboresha baadhi ya Barabara ambazo zimekuwa korofi