Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Wafanyabiashara wilaya Mpanda mkoani Katavi wameishutumu Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Katavi kuwa ni moja ya chanzo cha kufirisika kwa mitaji yao.
Wafanyabiashara hao wamebainisha hayo katika kikao kilichoandaliwa na mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ambapo wamesema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikiwatoza tozo kubwa kinyume cha sheria na pasipo kuzingatia ukubwa wa mitaji yao John benjamini anakuja na undani wa taarifa hii.
KATAVI – TANGANYIKA
Wakulima wa zao la Pamba kijiji cha vikonge kata ya Tongwe Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika wameiomba serikali kupitia Wizara ya kilimo kuongeza bei ya zao hilo.
Wakizungumza katika uzinduzi wa soko la Mauzo ya zao la Pamba katika kijiji cha vikonge wananchi hao wamesema changamoto ya kubadilika kwa bei imekuwa ikishindwa kuwanufaisha wakulima hao katika msimu wa mavuno – Mwanahabari Wetu BEN GADAU anao undani wa Taarifa hii.
MPANDA
Wamiliki wa kumbi za starehe na nyumba za Ibada Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia viwango vya sauti vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria ili kupunguza madhara ya kiafya yanayoweza kujitokeza kwa binadamu.
VERONICA MABWILE AMETUANDALIA TAARIFA IFUATAYO.
MPANDA.
Umaskini umetajwa kama chanzo moja wapo kinachopelekea watoto wa kike kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi kabla ya muda na kusababisha mimba za utotoni.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na mpanda redio fm na kusema kuwa umaskini na kipato duni cha familia ni chanzo cha mtoto wa kike kuingia kwenye mahusiano kabla ya umri WILLIAM LIWALI ana undani wa taarifa hiyo
MICHEZO
Mashindano ya UMITASHUMTA yametamatika mkoani hapa, mchezo wa Yanga na USM Alger waacha athari hasi kwa baadhi ya mashabiki, kimataifa Dontmund anyang’anywa tonge mdomoni na Bayern Munich.
Huyu hapa mwanamichezo wetu Killian Samwel na undani wa taarifa hizo.