skip to Main Content

KATAVI.

Wakulima Mkoani Katavi wametakiwa kuzitumia vizuri mvua zilizoanza kunyesha kwa kupanda mazao kwa wakati kuiga mbinu za kisasa za kilimo kama njia moja ya kuongeza mazao.

Rai Hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Beda Alfredy Katani alipokuwa akizunguza na kituo hiki kuhusu hali ya kilimo msimu huu.

Beda ameongeza kuwa kufuatia kubadilika kwa hali ya anga na pia kupungua kwa rutuba kwenye udongo, ni muhimu kutumia mbinu mpya za ukulima kwani mbinu za jadi hazina uwezo wa kutoa mazao mengi.

Kilimo ni eneo la kipaumbele katika uchumi wa Tanzania licha ya kuwa  kilimo nchini bado kinategemea kwa kiasi kikubwa mvua na hali ya hewa kwa ujumla .

Back To Top