skip to Main Content

MPANDA.

Mtoto wa Kike Mwenye Umri wa Miaka 3 Mtaa wa Rungwa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi amekutwa amefariki Dunia jana  Oktoba 4,2021 katika Kisima cha Maji.  

Akithibitisha Kifo hicho  Mwelela Nkokwa Mwenyekiti mtaa wa Rungwa amesema Mtoto huyo hakuonekana Nyumbani kwao kwa muda wa Siku 3.   

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Katavi Walifika na kuuopoa mwili wa mtoto huyo kisha kuondoka nao kwa uchunguzi zaidi huku Sajenti pastory Kikwala akitoa rai kwa jamii kufukia visima na mashimo marefu.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Katavi Rejina Kaombwe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Back To Top