skip to Main Content

GEITA. 

Mkazi wa kijiji cha Busanda kata ya Busanda wilayani Geita Unice Kulwa(25) na wanawe wawili wamepoteza maisha baada ya kukosa hewa kutokana na kuingiza  jiko la mkaa alilokuwa akipikia maharage kwenye nyumba waliyolala.

Mbali na vifo hivyo pia baba wa familia hiyo Kulwa Kamili amenusurika kifo na amelazwa kwenye kituo cha afya Katoro akiendelea kupatiwa matibabu.

Akielezea tukio hilo Ofisa mtendaji wa Kata ya Busanda Victoria Mapunda amesema mama huyo baada ya kumaliza kupika chakula cha usiku aliinjika maharage jikoni na kwenda kulala na saa tisa usiku mmoja wa majirani alihisi hali ya tofauti na  na alipotoka nje alikutana na hali ya tofauti.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 3,2021 katika kitongoji cha Shilungule kijiji cha Busanda wilayani humo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuacha tabia ya kuingiza jiko ndani huku wao wakiwa wamelala na kuchukua tahadhari za majanga mengine hasa wakati huu wa msimu wa mvua ikiwa ni kuhakikisha vyoo wanavyotumia ni imara.

Back To Top