Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
KATAVI
Waandishi wa Habari mkoani Katavi wamemuomba mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko kutatua changamoto zinazowakabili , ikiwemo kukosa bima ya afya, kukosa mikopo na kukosa ushirikiano kwa baadhi ya wakuu wa idara.
Wakizungumza mbele ya mkuu wa mkoa ,waandishi wa habari mkoani hapa alipowatembelea kwenye ofisi za umoja wa waandishi KTPC Katavi Press Club wamesema kuwa changamoto hizo zinafanya baadhi ya shughuli za kiuandishi kutofanyika kwa ufanisi.
Akijibu changamoto hizo mkuu wa mkoa amesema, anatambua mchango wa waandishi wa habari kwenye jamii hivyo ameahidi kuzitatua changamoto zinazowakabili .
Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa ameahidi kuwapatia waandishi wa habari pikipiki mbili zitakazo wasaidia katika kutekeleza majukumu ya kazi..