skip to Main Content

KATAVI

Vyombo vya ulinzi na usalama vimeagizwa  kushiriki kwa ukaribu zoezi la usajili wa  vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya katavi na rukwa .

kauli hiyo imetolewa na waziri wa katiba na sheria Palamagamba Kabudi katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kusema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinajukumu la kuhakikisha wote wanaosajiliwa wanasifa na wanastahili.

Sambamba na hilo Kabudi ametoa onyo kwa yeyote ambae atatoa taarifa za udanganyifu ili kujipatia cheti hicho atakuwa ametenda kosa la jinai na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Serikali imekuwa ikifanya zoezi la usajili wa vizazi  vifo na ndoa ikiwa na lengo la kufahamu taarifa sahihi za wananchi wake ili kupanga mipango bora ya kuwahudumia.

Back To Top