skip to Main Content

Tanganyika

Serikali wilayani Tanganyika mkoani katavi  imesema kuwa itaendelea kuchukua hatua  za kisheria ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa baadhi ya wananchi wanao vamia maeneo ya  hifadhi na mapitio ya wanyama.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya hiyo Onesmo Buswelu wakati akizungumza na mpanda radio fm na kusema kuwa lengo la kutengwa kwa maeneo hayo ni kuendelea kuzilinda rasilimali zilizomo katika eneo hilo

Aidha Buswelu amesema kuwa  wilaya hiyo ina maeneo mengi muhimu yanayohitaji ulinzi wa kila mwananchi ili kutokupoteza lengo la serikali la kuendelea kutangaza utalii katika wilaya hiyo.

Wilaya ya Tanganyika ni miongoni mwa wilaya zilizomo mkoani katavi zenye maeneo mengi yanayolengwa na serikali kuendelea kuweka matumizi bora ya ardhi kwa nia ya kulinda rasilimali zilizomo katika wilaya hiyo.

Back To Top