Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Wafanya biashara wa mtaa wa Shanwe kata ya Shanwe Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wanatarajia kuanza kufanya biashara juni mosi katika soko jipya, baada ya kupewa viwanja katika eneo la soko ililokuwa limetengwa kwa muda mrefu.
Wakizungumza na Mpanda Radio fm wamesema kwa muda mrefu wamekuwa na shauku ya kupata eneo linaloweza kuwakutanisha wafanya biashara wote, Awali walikuwa wakitumia vibanda majumbani kwaajili ya kutoa huduma na wameushukuru uongozi wa kata kwaajili ya kuwapatia ufumbuzi wa changamoto hiyo.
Akizungumza juu ya utaratibu uliotumika kugawa maeneo kwa wafanya biashara, mwenyekiti wa mtaa Shanwe Mustapha Kimasa amesema jumla ya viwanja 316 vimetolewa kwa wafanya biashara na wametenga eneo la kutupa taka, eneo la kujenga choo, na mfumo wa maji unaendelea kuletwa sokoni hapo.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Shanwe Hafidhi Makolokolo amesema kutokana na adha ambayo wamekuwa wakiipata wafanya biashara kupanga eneo la barabarani wakati wa usiku, wameona ni vyema watenge eneo kwa huduma za muda wakati wanasubiri mchoro rasmi wa halmashauri.