skip to Main Content

Dar es Salaam.

Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo imemsimamisha kazi Kaimu meneja wa uwanja huo, Said Mtumbuka na wafanyakazi wengine sita Kufuatia kukatika umeme uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wa mechi ya robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika, Kati ya Yanga na Rivers United.

Taarifa iliyotolewa Aprili 30 na wizara hiyo, imesema Waziri Dk Pindi Chana amemwagiza katibu Mkuu wa wizara hiyo hiyo, Said Yakubu kuwasimamisha watumishi wakiwamo aliyekuwa Mhandisi wa Umeme, Manyori Kapesa na aliyekuwa Afisa Tawala wa Uwanja huo, Tuswege Nikupala.

Aidha, rungu hilo limewapitia wafanyakazi wengine akiwemo, Gordon Mwangamilo, Gabriel Mwasele, Yanuaria Imboru na Dk Christina Luambano.

Taarifa hiyo imesema Katibu Mkuu wa wizara Said Yakubu amemteua Milinde Mahona kuwa Kaimu Meneja wa uwanja huo kuanzia Mei 1, 2023.

Kwa upande wao Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupitia taarifa yake rasmi iliyotolewa na kurugenzi yao ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma imesema haihusiki na kukatika kwa umeme katika uwanja huo.

Pia, wamesema baada ya majenereta kushindwa kufanya kazi katikati ya mchezo ndipo walitumia umeme wa Tanesco na mechi ikaendelea

Back To Top