skip to Main Content

DAR ES SALAAM. 

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Hayati Malkia wa Uingereza, Elizabeth II kilichotokea September 08,2022 nchini Uskochi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus inasema maombolezo hayo yataanza leo Jumamosi September 10, 2022 hadi September 14,2022, katika kipindi chote cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania zikiwemo kwenye Balozi

Rais Samia amewaomba Watanzania wote kuungana na wenzetu wa Uingereza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa Kiongozi wao nchini humo.

Back To Top