skip to Main Content

KATAVI

Vijana mkoani Katavi wameshauriwa kutofanya maamuzi mabaya  pindi wanapogubikwa na changamoto na badala yake waombe ushauri kwa watu wanaowazunguka.

Hayo yamesemwa na baadhi ya vijani mkoani hapa wakati wakizungumza na mpanda radio fm wamesema athari za matatizo ya kisaikolojia kiuchumi kwa kundi la vijana zimekuwa zikipelekea kijana kukata tamaa na kufanya maamuzi yasiyofaa huku wakitakiwa kuomba ushauri kwa watu wanaowazunguka.

.

Kwa upande wake mwanasaikolojia David amesema kijana mwenye matatizo ya kisaikolojia katika Nyanja ya kiuchumi anaweza kuathirika katika kufanya maamuzi na kuwa na tabia hatarishi kama ulevi na matumizi ya madawa ya kulevya.

.

David pia ameshauri vijana ambao wanakumbwa na changamoto hizo ni vema kufika katika huduma za unasihi ili kupata suluhisho.

Back To Top