Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
KATAVI
Miili ya watu 9 waliofariki katika ajali ya basi ya kampuni ya Kombas iliyotokea march 6 katika mlima Nkondwe halmashauri ya wilaya Tanganyika mkoani Katavi imeagwa katika hospital ya manispaa ya Mpanda .
Akizungumza wakati wa zoezi la kuaga miili hiyo mkuu wa wilaya ya Tanganyika onesmo Buswelu ametoa pole kwa waliofikwa na msiba huo ,pamoja na majeruhi wa ajali hiyo na kuwapongeza wananchi ambao wamejitokeza kuwasaidia wahanga wa ajali hiyo na kusema wamekuwa waaminifu katika zoezi hilo la uokoaji, huku akieleza mizigo iliyokuwa ndani ya bus hilo imehifadhiwa katika kituo cha polisi cha kibo.
Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Hoza mrindoko ametoa pole kwa familia zilizoguswa na msiba huo ,pamoja na majeruhi wa ajali hiyo na kueleza juu ya hatua za serikali ilizochukua kutokana na ajali hiyo.
Mrindoko amesema miili saba imetambulika na ndugu zao lakini miili miwili bado haijatambulika na kuvitaka vyombo vya habari na wananchi kuendelea kutoa taarifa ili miili hiyo iweze kutambuliwa na ndugu zao.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Katavi ametoa salamu za pole kutoka kwa raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassain kwa kuwapa pole wafiwa na kuwaombea majeruhi wa ajali hiyo kupona haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao kama kawaida.