miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
KATAVI
Watu Wenye ulemavu Mkoani Katavi wameshauriwa kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia mbili inayotolewa na serikali kupitia halmashauri zote nchini.
Katibu wa Chama cha watu wenye ulemavu Mkoa wa Katavi Godfrey Sadala ameiambia Mpanda Radio kuwa watu wenye ulemavu wanahofia kwenda kufuatilia fedha za Serikali kwa kuhofia marejesho kuwataka kujitokeza kuomba mikopo hiyo.
Kwa upande wao baadhi ya watu wenye ulemavu wamesema kuna changamoto ya ufuatiliaji wa mikopo hiyo na kuwashauri wenzao kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo ili kujikwamua kiuchumi.
Katika Bajeti mpya ya Mwaka 2023/2024 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amezisisitiza Halmashauri Zote mkoani hapa kuendelea kutenga asilimia 10 kwa ajili ya mahitaji ya Vijana Wanawake na watu wenye Ulemavu.