Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
NSIMBO
Baadhi ya wananchi wametoa maoni mseto kutokana na tukio la mtoto mchanga kutupwa katika shimo la choo kitongoji cha Isagala kijiji cha Uruwila Hamshauri ya Nsimbo Mkoani Katavi.
Wakizungumza na Mpanda Redio Fm kwa nyakati tofauti wameviomba vyombo vya dola kuchukua hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kutokana na kukithiri kwa matukio ya aina hiyo ya ukatili.
Kwa upande wake afisa ustawi halmashauri ya Nsimbo Theresia Mwendapole amekiri kumpokea mtoto huyo huku akisema tayari amekwisha patiwa matibabu na kwa sasa anaendela vizuri kiafya.