Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MLELE
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza halmashauri ya wilaya ya mlele katika makusanyo ya mwezi wa 10 hadi 12 waanze ujenzi wa shule nyingine ya sekondari ili kupunguza mlundikano wa wanafunzi uliopo katika shule ya sekondari Majimoto.
Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari majimoto amewataka wataalamu kuhakikisha wanatumia mapato ya halmashauri kwa manufaa ya wananchi na sio posho peke na kupendekeza shule iitwe Majimoto B.
Aidha Majaliwa amewataka wananchi kupendekeza eneo ambalo wanahitaji ujenzi wa shule hiyo kufanyika na ameongeza kuwa watumishi wa serikali na viongozi wasibweteke na kutegemea pesa za serikali pekee bali watoe katika mapato ya halmashauri.
Ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ilianza rasmi tarehe 12/12/2022 na kuhitimishwa 14/12/2022 ambapo amekagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo na uwekaji wa mawe ya msingi na uzinduzi wa kiwanda cha maziwa MSS mkoani hapa.