skip to Main Content

KATAVI
Waziri Mkuu Wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa amesema kiasi cha fedha cha shillingi Bilioni 150 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ruzuku ya pembejeo kwa wakulima ili wapate mbolea na dawa Mkoani Katavi.

Ameyasema hayo alipokuwa katika ziara yake na kuzungumza na wananchi katika kijiji cha kagunga kilichopo wilayani Tanganyika ambapo Amesema zaidi ya tani 4954 za mbolea zimetengewa kwa ajili ya mkoa wa Katavi.

Aidha Majaliwa amewataka viongozi wenye dhamana kuhakikisha wanasimamia vyema ili pembejeo ziweze kuwafikia wakulima Kwa wakati.

Ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa imeanza tarehe 12 na inatarajia kumalizika tarahe 14 december 2022 huku ikiambatana na ukakuguzi wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo mkoani hapa.

Back To Top