Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MLELE
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kuangalia upya utolewaji wa vibali vya ukataji miti ili kuthibiti ukataji miti na kutunza mazingira.
Akizungumza na watumishi wa umma katika halmashauri ya wilaya ya mlele na kusema kuwa serikali inathibiti uharibifu wa mazingira lakini Wakala wa huduma za misitu Tanzania[Tfs ] wanatoa vibali vya ukataji miti hali ambayo inaleta uharibifu wa mazingira.
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amewataka Tfs kuangalia upya utolewaji wa vibali vya ukataji miti ili kuthibiti uharibifu wa mazingira.
Ziara ya siku tatu ya waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania imelenga kutembelea Miradi mbalimbali ya kimaendeleo sambamba na kuzungumza na wananchi pamoja na watumishi wa umma ambapo imeitimishwa tarehe 14 december 2022.