Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
KATAVI
Baadhi ya wakulima mkoani Katavi wasema wanahofia kuanza kupanda mazao katika mashamba yao kutokana na hali ya hewa ilivyokwasasa tofauti na miaka mingine.
Wakizungumza na Mpanda radio fm kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa katika miaka ya nyuma imezoeleka tarehe za miezi kama hii baadhi ya mazao huwa tayari yameota na kufikia hatua ya kupaliliwa lakin kutokana na mabadiliko ya tabianchi mpaka sasa mvua bado hazijanyesha na kumekuwa na ongezeko la joto.
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ilitabiri ongezeko la vipindi vya joto kali kuendelea kujitokeza katika mwezi Novemba 2021 na kupungua kidogo ifikapo Disemba 2021, ambapo mtawanyiko wa mvua unatarajiwa kuongezeka sambamba na mionzi ya jua la utosi kuwa imeondoka katika maeneo ya nchi yetu. Aidha kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP imesema takribani mataifa 43 yapo hatarini kukabiliwa na baa la njaa duniani huku miongoni mwa sababu zinazotajwa ni athari za mabadiliko ya tabia nchi.