skip to Main Content

KATAVI.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Beda Alfredy Katani amemuomba Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kupitia  uamuzi wake wa kubadilisha umiliki wa Misitu ya Tongwe Mashariki na Tongwe Magharibi kutoka Halmashauri hiyo kwenda TAWA.

Beda ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Mpanda Redio kutokana na kuwa Msitu huo uko chini ya Halmashauri hiyo toka Mwaka 1963 na haoni sababu za kubadilisha misitu hiyo.

Aidha Beda ameishauri serikali kurasimisha vijiji ambavyo vipo ndani ya wakala wa misitu Tanzania ii kwendana na uhitaji wa ardhi kulingana na ongezeko la idadi kubwa ya watu.

Tarehe 25 mwezi wa 6 mwaka huu Raisi wa Tanzania Samia suluhu hasani alisaini tangazo / nyaraka ambayo unawamilikisha mamlaka ya usimamizi wanyamapori Tanzania  TAWA Kwenda kusimamia Misitu ya Tongwe Mashariki na Tongwe Magharibi.

Back To Top