Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
KIMATAIFA
Mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na WhatsApp ilisita kufanya kazi kwa masaa kadhaa tangu jana jioni, lakini hatimaye kwa kiasi fulani imeanza kufanya kazi tena saa chache zilizopita.
Kampuni ya Facebook inayomiliki majukwaa mengine mawili ya Instagram na WhatsApp imetangaza kuwa imeanza kuishughulikia hitalifu hiyo muda mfupi baada ya kujitokeza.
Siku ya Jumapili mfichuwa udukuzi mmoja aliishutumu Facebook kwa kuweka mbele faida kuliko kushughulikia tatizo la matamshi ya chuki na taarifa za uongo zinazosambazwa kwenye jukwaa hilo.
Kufuatia ripoti hiyo hisa za Facebook zilianguka kwa asilimia 5.3 ilipofika Jumatatu, Wataalam wa usalama wanasema linaweza kuwa ni tatizo la kiufundi au inawezekana kuwa ni hujuma iliyofanywa na mfanyakazi wa ndani ya kampuni hiyo.