Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Halmashauri ya manispaa ya mpanda mkoani katavi imetenga shilingi milioni mia moja kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa shule ya sekondari nsemulwa kabla ya kufika mwaka 2022.
Kauli hiyo imetolewa na meya wa manispaa ya mpanda Aidary Sumry alipokuwa kwenye ziara ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya manispaa na kueleza mikakati waliyonayo ili kufanikisha kupokea wanafunzi ifikapo mwaka 2022.
Kwa upande wake afisa elimu sekondari manispaa ya mpanda Enelia Lutungulu ameeleza kuwa shule ya sekondari nsemulwa ikikamilika itaondoa changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu.
Kata ya Nsemulwa haina shule ya sekondari licha ya sera ya elimu nchini inataka kuwa na shule ya sekondari kila kata.