skip to Main Content

MPANDA

Mstahiki meya wa manspaa ya Mpanda Haidary Sumry amewaagiza madiwani kufuatilia fedha zinazopitishwa kwenye miradi ya maendeleo ili kukamilika kwa wakati.

Akizungumza katika baraza la madiwani amesema ufuatiliaji huo utasaidia kiwango Cha pesa zinazoelekezwa kwenye miradi kuendana na kasi ya utekelezaji.

Katika hatua nyingie Baraza la madiwani limempongeza Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha    kwaajili ya kukamilisha miradi ya maendeleo ikiwemo fedha za makato ya simu.

Fedha zilizotolewa zimetengwa kwaajili ya kujenga vyumba madarasa 59 katika halmashauri ya manspaa ya Mpanda huku fedha nyingine zimepangwa katika ujenzi wa kituo cha afya Nsemulwa.

Share
Back To Top