miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
baadhi ya vipimo vya kimaabara .picha na mtandao
Na Samweli Mbugi -Katavi
Wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuwapeleka Watoto wenye selimundu hospitali kwa ajili ya matibabu na ushauri kwani ugonjwa huo sio wakuambukizwa bali ni wa kurithi .
Hayo yamesemwa na kaimu mganga mfawidhi hospitali ya manispaa ya Mpanda Dkt Mundhiri Bashiru wakati akizungumza na Mpanda redio fm ameongeza kuwa kutokana na ukosefu wa elimu wananchi wamekuwa na Imani potofu juu ya ugonjwa huo.
Katika hatua nyingine amesema waathirika wakubwa ni kuanzia mtoto wa umri wa miezi sita na kuendelea na moja ya dalili ni maumivu kwenye vidole na maeneo mengine na kuishiwa damu mara kwa mara
Baadhi ya wananchi wameeleza uelewa wao juu ya ugonjwa wa selimundu na ni kwa namna gani unahatarisha maisha endapo hautapata tiba ya hospitali huku wakionyesha kutokuwa na uelewa wa chanzo cha ugonjwa huo
Maadhimisho ya mwaka huu yamekwenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘Vunja mduara ,pima, jua hali yako ya sikoseli.