skip to Main Content

Picha na mtandao

Na Samwel Mbugi -Katavi

Mtoto mwenye umri wa miaka 8 ambae jina lake limehifadhiwa kutoka Kijiji cha Dirifu Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi inadaiwa kalawitiwa na kijana aliyejulikana kwa jina moja la Shingisha.

Akizungumza na Mpanda Radio Fm Mlezi wa mtoto huyo ambae ni babu yake,  jina lake limehifadhiwa, amesema kuwa baada ya kupata taarifa hizo amefanya jitihada za kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha polisi,hospital ili kupata matibabu na hatua nyingine za kisheria

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Msangama Kijiji cha Dirifu Regna Josephat Salia amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kueleza ni  tukio la nne kutokea katika kitongoji hich

Nae Tabibu wa Magonjwa ya inje (OPD) kutoka Hospital ya Manispaa ya Mapanda mkoa wa Katavi Godfrey Bartazali amethibitisha kupokea Mtoto huyo na kumfanyia vipimo ambavyo vilithibitisha kuwa amefanyiwa ukatili huo.

Mpanda Radio Fm inaendelea kumtafuta kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi kwa ajili ya ufafanuzi zaidi wa tukio hilo.

Back To Top