Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
TANGANYIKA.
Wananchi wa halmashauri ya Tanganyika wametakiwa kuiunga mkono serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu ili kumsaidia mtoto wa kike kupata elimu bora.
Wakizungumza na Mpanda redio fm baadhi ya wananchi wametaja kuwa ubovu wa miundombinu shuleni ni moja ya sababu ambayo huwafanya baadhi ya watoto wa kike kukatisha masomo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanganyika Juma J shabani amesema kuwa kukosekana kwa miundombinu bora shuleni humuathiri binti kisaikolojia sambamba na kukatisha masomo huku akiendelea kuwaasa wananchi kushirikiana na serikali katika kuboresha miundombinu hiyo.
Kwa mujibu wa takwimu za elimu za taifa (BEST) za mwaka 2016,ni asilimia 43.6 tu ya shule za msingi na asilimia 54.4 ya shule za sekondari nchini ndizo zenye huduma hiyo.