skip to Main Content

KATAVI

Wananchi wa Kayenze Kata ya Katuma Halmashauri ya Tanganyika mkoani Katavi wamewaomba Wakala wa barabara Vijijini TARURA kurekebisha Barabara ya Sibwesa Katuma inayopita katika eneo lao.

Wameiambia Mpanda Radio kuwa wanapata adha ya usafiri na kushindwa kufanya baadhi ya majukumu Kutokana na ubovu wa barabara na baadhi ya maeneo vifusi vimemwagwa na bila kutawanywa.

Vicent Kadogosa , Mwenyekiti wa Kayenze B ameiomba Serikali kuwahimiza Wakandarasi kuweka kifusi kizuri ambacho kitaimarisha barabara huku akiwasihi wafugasi kupitisha mifugo yao kwenye njia walizokubaliana.

Akazingumzia suala hilo Diwani wa Kata ya Katuma Bwana Paulo Pomasi amesema kuwa usimamaizi hafifu wa Mkandarasi wa kutoka Sibwesa hadi Kayenze ndio umepelekea barabara kutokuwa imara.

Juhudi za Kumpata Meneja wa TARURA wa Halmashauri ya Tanganyika Bwana Nolassco zinaendelea.

Back To Top