skip to Main Content

MPANDA
Takwimu zinaonyesha kwa mwaka 2022 wagonjwa wapya 21 wamebainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa ukoma ndani ya manispaa ya mpanda mkoani katavi hali inayoonesha uwepo mkubwa wa watu wenye tatizo hilo.

Kauli hiyo imetolewa na mratibu wa kifua kikuu na ukoma manispaa ya mpanda Bruno Cronery wakati wa kipindi cha afya ya jamii kinachoruka katika kituo hiki na kueleza kuwa ugonjwa huo unatibika.

Kwa upande wake mganga mfawidhi kituo cha afya Nsemulwa daktari Herman Kimango ameitaka jamii kuondokana na imani potofu juu ya ugonjwa huo na kusema kuwa ukoma ni ugonjwa unaoambukizwa kwa hewa huku akizitaja dalili zake kuwa ni kutokwa madoa yasiyo na rangi katika mwili.

Dunia huazimisha siku ya ukoma kila ifikapo jumapili ya mwisho wa mwezi January kwa kila mwaka.

Back To Top