Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Jumla ya wanafunzi wa kike 45 walio katishwa masomo kwa sababu mbalimbali wamesajiliwa kufanya mitihani ya kidato cha pili na cha nne katika kituo cha Kashato TRC ambapo wakidato cha pili ni 32 na kidato cha nne ni 13.
Hayo yamesemwa na Fisia Patrick Konzo afisa elimu kata ya makanyagio wakati akizungumza na mpanda redio fm Ambapo amesema wanafunzi hao wamesajiliwa kwa ajili ya kufanya mitihani yao ya kidato cha pili na channe mwaka huu huku akianisha changamoto na kuishauri jamii kuwapa nafasi wapate haki ya elimu.
Kwaupande wao wanafunzi ambao wamesajiliwa kufanya mitihani hiyo wameahidi kufanya vizuri katika masomo yao ili waweze kutimiza ndoto zao na kuwashauri wanafunzi ambao bado hawajajiunga watumie fursa hii ili kupata haki ya msingi ya elimu.
Kila mtoto anayo haki ya kupata elimu jamii eendelee kuwapeleka watoto shule ili waweze kupata haki yao ya kupa elimu.