skip to Main Content

KATAVI

Mtu mmoja anayefamika kwa jina la Aden Mwakipesile mwenye umri wa miaka 49 mkazi wa kijiji cha Ibindi wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi amekutwa amefariki kwa kujinyonga nyumbani kwake usiku wa kuamkia April 4.

Mke wa marehemu Letisia Deus ameeleza jinsi tukio la kujinyonga kwa mume wake lilivotokea huku akishitushwa na maamuzi ya mume wake kwa kufanya tukio hilo.

Kwa upande wao majirani wa marehemu wamesema tukio hilo limewashitua na kwamba tukio la mtu kujinyonga ni kwa mara ya kwanza kutokea kijijini hapo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Ally Makame Hamad amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiitaka jamii kutofanya maamuzi ya kujiondoa uhai.

Back To Top