Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Wafanya biashara wa soko la Mpanda hotel manisapaa ya Mpanda Mkoani Katavi wanaouza matunda ya msimu nje ya soko, wamelalamikia ushuru wanaotozwa na kuomba kupewa ruhusa ya kuuza biadhaa nyingine ambazo sio za msimu nje ya soko.
Wameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika sokoni hapo na kusema baadhi ya wafanya biashara wamekuwa wakishindwa kuwaletea bidhaa kwa kuogopa ushuru ambao haulingani na mizigo, na wengine wamekua wakitozwa mara mbili, sambamba na kupewa ridhaa ya kuuza mazao mengine eneo hilo ambayo sio ya msimu.
Akijibia hoja hizo mwenyekiti wa soko Elisha Joseph Kang`ombe amesema kuwa kuhusu swala la kutoza ushuru watashughulukia kuhakikisha tozo zinaligana na mizigo, na kuhusu suala la kuuza nje mazao ambayo sio ya msimu amekataa na kupiga marufuku kwani bidhaa hizo zimnatakiwa kuwa ndani ya soko.
Aidha amesema suala la kutozwa ushuru zaidi ya mara moja kwa wafanya biashara wa ndizi ameshalifikisha kwa mkurugenzi na afisa biashara ili kuwaepushia changamoto wafanyabiashara wa ndizi ambao wamekuwa wakikumbana na changamoto hiyo.