skip to Main Content

KATAVI
Uwepo wa Wadhamini wa kilimo katika mkoa wa katavi utasaidia ukuaji wa maradufu wa tija ya uzalishaji katika mazao mkoani hapa.

Akiongea katika kongamano la Wadau wa Sekta ya Kilimo wa Pass Trust kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko, katibu Tawala msaidizi Nehemia James amesema kuwa umuhimu wa Pass Trust unasaidia katika suala la Kukopa huku ukisaidia kwa Benki kuwa na uamuzi wa kukopesha Wadau.

Aidha Meneja Maendeleo ya Biashara wa pass Trust Bwana Herman Bashiri amewaomba wadau wachangamkie fursa zilizopo katika katika kijani shirikishi.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wamefurahishwa na hatua ya Pass trust kuwapa fursa ya Mikopo na kutoa somo la kuwasaidia wakulima katika uzalishaji wa Tija.

Pass Trust ambayo imelenga kukijanisha maisha katika ukuaji wa Uchumi wa Kijani Shirikishi inagusa udhamini hadi wa asilimia themani kwa miradi ya Kilimo inayochochea ukuaji wa uchumi ina fanya kazi kwa uzoefu wa miaka 23 kwa sasa.

Back To Top