skip to Main Content

KATAVI
Ukatili wa kingono umetajwa kuwa ni chanzo kimoja wapo cha mimba za utotoni Mkoani Katavi ambapo jamii imehaswa kuwalinda watoto.

Hayo yamesemwa na afisa maendeleo ya jamii Joshua Sankala alipokuwa kwenye uzinduzi wa siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo ameseme kwa mwaka huu mimba za utotoni zimeongezeka.

Aidha Joshua amesema hali ya mimba za utotoni kwa siku za hapo nyuma haikuwa kubwa sana ukilinganisha na mwaka huu.

Uzinduzi wa kupinga ukatili wa kijinsia umefanyika 25 november mkoani hapa na utahitimishwa December 10 mwaka 2022,huku kauli mbiu ikisema kila uhai unathamani ,tokomeza mauaji na ukatili wa wanawake na watoto.

Back To Top