skip to Main Content

MPANDA
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoani Katavi Idi Hassan Kimanta amesema Mahusiano bora baina ya wafanyabiashara na mamlaka ya mapato [TRA] mkoani Katavi ni sababu ya Kuwa kinara katika ukusanyaji bora wa mapato.

Amesema Hayo wakati wa kilele cha wiki ya mlipa kodi hivi karibuni na kuainisha kumekuwa na umoja wa viongozi wa pande hizo mbili na kuwataka kuendelea ili kusaidia kukuza uchumi.

Amani Mahela Mwenyekiti wa jumuia ya wafanyabiashara mkoa wa Katavi amewaomba wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi kuacha ili kuleta maendeleo kwa nchi pia mamlaka kuendelea kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara wapya

Katika hatua nyingine Kimanta ametoa wito kwa wananchi pamoja na wafanyabiashara kutoa na kudai risiti wanapouza na kununua bidhaa ili kuchangia mapato na uchumi kwa nchi.

Back To Top