Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Wananchi wa kitongoji cha Bwawani mtaa wa Kigamboni wanaoishi pembezoni mwa bwawa la Milala wamelalamikia ucheleweshwaji wa fidia na taarifa kuhusu makazi yao, ambayo walisimamishwa kufanya shughuli zote za kimaendeleo.
Wakizungumza na Mpanda Radio fm wananchi hao wamesema kuwa tangu ilipopita kamati ya mawaziri kufanya mapitio ya mipaka na kuwasimamisha kufanya shughuli za uendelezaji wa makazi katika eneo hilo, bado hawajui hatima ya maisha yao licha ya jambo hilo kuchukua takribani miezi kumi bila taarifa yeyote.
Akijibia changamoto hiyo mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza mrindoko amekiri kuwa jambo hilo limechukua muda mrefu, licha ya wananchi kusimamishwa kufanya shughuli katika eneo hilo, ambapo amesema majukumu waliokabidhiwa na kamati ya mawaziri, wao kama mkoa wameshakamilisha na kutuma mrejesho wizarani ambapo wanatarajia kupokea majibu hivi karibuni.
Aidha Mwanavua amewataka wananchi wanaoishi katika mazingira yanayozunguka katika eneo hilo, kuwa wavumilivu licha ya suala hilo kuchukua takribani miezi kumi bila kuwa na mrejesho.