skip to Main Content

TANGANYIKA

Mwenge wa uhuru unatarajia kuzindua na kutembelea miradi saba yenye thamani Zaidi ya bilioni 1.9 katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amebainisha kuwa mwenge wa uhuru unatarajiwa kuwasili wilayani hapo tarehe 24 ya mwezi huu ukitokea mkoani Kigoma na utaweza kuzindua mradi wa maji vikonge,kukagua barabara ya kasekese na kuwaomba wananchi kujitokeza kuulaki mwenge wa uhuru

Meneja wa mamlaka wa maji Ruwasa Alkam Sabuni na meneja wa wakala wa bara bara za mjini na vijijini wilaya ya Tanganyika tarura injinia Nolasco Kamasho wamesema kuwa katika miradi ambayo mwenge wa uhuru utafanya ukaguzi na kuzindua miradi hiyo ni moja ya miradi ambayo inakwenda kuwasaidia wananchi na imekidhi viwango kuzinduliwa na mwenge wa uhuru

Mwenge wa uhuru inatajia kuingia mkoan Katavi tarehe 24 ya mwezi huu ukitokea mkoani Kigoma huku mbio za mwenge wa uhuru ikiwa na kauli mbiu isemayo “Tunza mazingira, Okoa vyanzo vya maji kwa Ustawi wa viumbe hai kwa uchumi wa Taifa

#mpandaradiofm97.0

#mwenge

Back To Top