miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
DAR ES SALAAM.
Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania, kimependekeza mikutano ya hadhara iruhusiwe sambamba na mabadiliko ya sheria mbalimbali zitakazowezesha mikutano hiyo kufanyika kwa ufanisi.
Hayo yamebainishwa Ikulu jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa kikosi kazi, Profesa Rwekaza Mukandala wakati akiwasilisha mapendekezo ya kikosi hicho kwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema baada ya kikosi hicho kufanya kazi kwa miezi 10 kikichambua maoni mbalimbali ya wadau, kinapendekeza kwamba mikutano ya hadhara iliyozuiliwa mwaka 2016, iruhusiwe kufanyika.
Mwenyekiti huyo amesema kikosi kazi kinapendekeza Sheria ya Vyama vya Siasa ifanyiwe marekebisho ili kulipatia Baraza la Vyama vya Siasa mamlaka ya kushughulikia uvunjifu wa maadili ya vyama vyenyewe
Pia, kuweka idadi ya jinsi moja ndani ya vyama vya siasa isipungue asilimia 40. Amesema marekebisho hayo yaangazie pia ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika shughuli za chama husika.