miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
picha na Mtandao
KATAVI
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Doto Biteko, amewataka wasimamizi wa mradi wa umeme wa gridi yaTaifa mkoani Katavi kuacha visingizio na kuhakikisha mradi huo unakamilika ifikapo Oktoba mwaka huu.Dkt. Biteko ameyasema baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa njia kuu ya kusafirisha umeme kutoka Tabora hadi Katavi na kituo cha kupokea na kusambaza umeme kilichopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ambapo kituo hicho kwasasa kimefikia asilimia 63.
Dkt. Biteko ameyasema baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa njia kuu ya kusafirisha umeme kutoka Tabora hadi Katavi na kituo cha kupokea na kusambaza umeme kilichopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ambapo kituo hicho kwasasa kimefikia asilimia 63.
Naye Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza thamani ya uchakataji wa mazao viwandani.
Katavi unatumia umeme unaozalishwa kwa mafuta na mashine za jenereta ambao haukidhi mahitaji ya wananchi na kupelekea changamoto ya kukatika mara kwa mara.