miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
TANGANYIKA
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu ametoa maelekezo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Tanganyika kuangalia namna bora ya ukusanyaji wa mapato katika kipindi hiki cha mavuno.
Maelekezo hayo ameyatoa wakati wa kikao cha baraza la madiwani wilaya ya Tanganyika ambapo amesema kumekuwa na mianya mingi ya utoroshaji wa mapato jambo ambalo linapelekea halmashauri kutokuwa na mapato ya kuridhisha.
Akichangia hoja ya Mkuu wa Wilaya, Getruda Kilembe Diwani viti maalum Kata ya Kesekese ameomba wakatisha ushuru walipwe malipo kwa wakati ili kuepusha ushawishi wa kuiba mapato wanayoyakusanya.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya Tanganyika Shaban Juma ameeleza mikakati ambayo wataitekeleza halmashauri ya wilaya ya Tanganyika katika kuziba mianya ya kupoteza mapato ikiwemo kuwawajibisha wakatisha ushuru wazembe.