skip to Main Content

KATAVI

Katika kuelekea sikukuu ya Eid El Fitri Jeshi la polisi mkoa wa Katavi limepanga kuimarisha ulinzi ili kupunguza uvunjifu wa sheria kipindi cha sikukuu.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Katavi Ali Makame Hamad amesema kuwa jeshi limejipanga vema kuimarisha ulinzi na kutakuwa na askari wa doria na kutakuwa na vikundi maalumu vitakavyofuatilia mienendo yote ya matukio mitaani hivyo wananchi washerekee sikukuu kwa amani na utulivu.

Aidha Makame wamewataka wazazi na walezi kuwa makini na Watoto na kutowapelekea katika kumbi za starehe huku akitoa angalizo kuwa hatua zitachukuliwa kwa wamiliki wa kumbi za wataowaruhusu Watoto walio na umri chini ya miaka 18 kuingia katika kumbi za starehe.

Jeshi la polisi mkoa wa Katavi linatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu na kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi ili kuweza kuwafichua watu wenye mienendo au viashiria vya kiharifu.

Back To Top