Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Kiongozi wa upinzani nchini ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa chama cha ACT wazalendo akizungumza na wananchi Katavi
Na John Mwasomola -Katavi
Kiongozi wa upinzani nchini ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa chama cha ACT wazalendo ametembelea kijiji cha Luhafwe Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi .
Kiongozi huyo amekutana na kero ya wananchi kudai kuhamishwa eneo hilo la luhafwe kwa ajili ya kupisha wawekezaji 26 ambao wanataka kulima kilimo cha mbegu za kisasa za alizeti na mahindi ambapo wao hawatambuliki kama ni wanakijiji au kata lakini wamekuwa wanatozwa fedha na kulipa kodi .
Akiwasilisha hoja hiyo mmoja wa wananchi amebainisha kuwa wamezunguka ofisi mbalimbali za viongozi wa chama cha CCM mpaka mkoa na kwa viongozi wa serikali bila kupata msaada hivyo wanaona chama cha ACT wazalendo kitawapa msaada .
Akijibu kero hiyo Zitto Kabwe amesema wananchi wasiwe na shaka kuhusu hilo ameahidi kwenda kulifanyia kazi na hakuna mwananchi atakayehama eneo hilo.
Ikumbukwe kuwa katika ziara hiyo wananchi wa kaya mianane wameamua kurudisha kadi za chama cha mapinduzi ccm na kuhami