skip to Main Content


Na John Benjamin- Katavi

Wafanyabiashara manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia adha ya kukatika kwa umeme mra kwa mara hali ambayo inawasababishia hasara

Hayo yamebainishwa na wafanyabiashara wakati wakizungumza na Mpanda Redio FM kwa nyakati tofauti na kueleza kuwa  Uchumi wao unayumba kutokana na shughuli zao kuhitaji umeme.

Akizungumza kwa njia ya simu afisa mahusiano wa shirika la umeme Tanzania mkoa wa Katavi Proches Joseph amesema kuwa kumekuwa  na maboresho kwa baadhi ya laini ya nishati hiyo  ya umeme.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo maboresho yanayofanyika  ni kwa ajili ya maandalizi ya mapokezi ya umeme wa  gridi ya taifa mwezi ujao

Back To Top