Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
KATAVI
Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya dereva bodaboda yaliotokea Julai 24 mkoani Katavi.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amesema watuhumiwa hao baada ya kutekeleza mauaji walichukua pikipiki ya marehemu na kutokomea kusikojulikana.
Baada ya Jeshi la Polisi kupokea taarifa hizo lilianza msako mkali na hatimaye kuzaa matunda kwa kuwakamata watuhumiwa na kuonyesha walipouzia pikipiki hiyo.
Kwa upande wao baadhi ya madereva bodaboda Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamesema wizi wa pikipiki umekua kero kwao huku wakilishukuru Jeshi la Polisi kwa kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.
Kamanda Ngonyani amesema watuhumiwa hao bado wanaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao mzima wa wizi wa pikipiki katika mkoa wa Katavi na mara baada ya mahojiano watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.