skip to Main Content
Moja ya vyanzo vya maji. Picha na Leah Kamala

Na Leah Kamala

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameeleza  madhara  katika mazingira endapo  vyanzo vya maji vitaharibiwa.

Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa madhara hayo yanaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji wa umeme pamoja na kuongezeka kwa magonjwa hivyo wameiomba serikali iendelee kutoa elimu ili kuepukana na madhara hayo.

Sauti za wananchi

Naye Afisa Mazingira Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Zaituni Rashid amewaelezea wananchi juu ya umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji ili kuhakikisha upatikanaji wa maji safi pamoja na kudumisha mazingira na ustawi wa viumbe hai

Sauti ya afisa mazingira

Ni muhimu kwa jamii, serikali na taasisi mbalimbali kushirikiana kulinda vyanzo vya maji kwa ajili ya uzalishaji wa chakula na kuhifadhi mazingira

Back To Top