skip to Main Content

Wajumbe wa kikao cha jukwaa la vijana la kilimo katika ukumbi  wa LATCU uliopo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.picha na Lilian Vicent

KATAVI

Vijana mkoani Katavi wameshauriwa kutumia sekta ya kilimo kama  fursa kupitia  majukwaa ya kilimo  .

Rai hiyo imetolewa na  Faridu Mtiru  Afisa kilimo mkoa wa katavi kwenye kikao cha jukwaa la vijana la kilimo katika ukumbi  wa LATCU uliopo manispaa ya Mpanda mkoani hapa   .

Katika hatua nyingine Mtiru amesema  kuwa vijana walioshiriki katika kikao hicho wanajihusisha na sekta ya kilimo hivyo watasaidia kuondoa mitazamo hasi iliyopo kwa  baadhi ya vijana  kuhusiana na  sekta ya kilimo.

Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii kutoka halmashauri ya wilaya ya mlele pamoja na baadhi ya wajumbe walioshiriki wamebainisha kuwa kupitia jukwaa hilo wanatarajia vijana wataendea kuhamasika kuingia kwenye sekta ya kilimo.

Kikao hicho cha jukwaa la vijana la kilimo kimehudhuriwa na wajumbe ambao ni vijana wanaojihushisha na sekta ya kilimo, maafisa kilimo pamoja na maafisa maendeleo  kutoka halmashauri mbalimbali..

Back To Top