skip to Main Content

MPANDA

Baadhi ya wazazi na walezi halmashuri ya manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametoa Maoni ya usafi wa vyoo katika shule za msingi na kuomba serikali kuendelea kusimamia ili kuwanusuru wanafunzi na magonjwa ya kuambukizwa ikiwemo UTI.

Wakizungumza na kituo hiki wamesema kuwa hali ya usafi wa mazingira pamoja na vyoo si ya kulidhisha jambo ambalo wamesema linarudisha nyuma maandeleo ya baadhi ya watoto kwa kuwa watoro huku wengine wakipata magonjwa ya kuambukizwa

Akizungumza kwa njia ya sim afisa habari wa Halmashauri ya Manispaa Mpanda Donald Pius amesema miongoni mwa vitu vinavyo mhamasisha mwanafunzi kuendelea kuhudhuria masomo ni pamoja na mazingira kuwa safi nakuwataka walimu wakuu kuhakikisha usafi wa vyoo unasimamiwa ipasavyo.

Back To Top