miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
MPANDA
Utekelezaji wa sheria ya kutofanya shughuli za kibinaadamu ndani ya mita 60 kutoka mtoni umekuwa bado una changamoto kwa wakazi wanaoishi karibu na maeneo ya mito licha ya msisitizo kuhusu sheria hiyo.
Baadhi ya wakazi wanaoishi kuzunguka mto Mpanda katika eneo la Misunkumilo wamesema kuwa wengi wao wanayatumia maeneo hayo katika kufanya shuguli mbalimbali ambazo zinawasaidia kupata kipato kama kilimo cha bustani kuosha pikipiki na magari na ufyatuaji wa matofali wakati wa kiangazi.
Kwa upande wake mwenyekiti mtaa wa Misunkumilo amesema kuwa kumekuwa na ugumu kwa watu kutii sheria hiyo licha ya kazi zinazofanywa na wananchi hao kuzunguka maeneo ya mito haziruhusiwi .
Mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya mpanda Sophia kumbuli hivi karibuni aliwaagiza watendaji kuhakikisha sheria ya kutofanya shuguli za kibinadam ndani ya mita 60 inafuatwa huku akisisitiza maeneo ya misunkumilo bado changamoto ya utekelezaji wake ni tatizo.