miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…

“Mrindiko ameagiza kuhakikisha malengo ambayo yanapangwa yanafikiwa Kwa wakulima kufuata mbinu za kilimo, na wataalamu kuhakikisha tathimini inafanyika ili kulinganisha na misimu mingine na kwanini imekuwa vigumu kufikia lengo la kuzaliza Tani milioni 50″ Picha na Festo Kinyogoto
Na Festo kinyogoto-katavi
Wakulima wa zao la Pamba tumbaku na mazao mchanganyiko Mkoani katavi wamehakikishiwa soko la Uhakika la mazao hayo pamoja na malipo Kwa wakati Ili kujikimu na kukuza uchumi.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa katavi Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindiko Katika hafla ya uzinduzi wa msimu wa masoko ya Pamba, tumbaku na mazao mchanganyiko iliyofanyika Katika kijiji Cha Makongoro kata ya Magamba halmashari ya Manisapaa ya Mpanda Mkoani katavi.
Mrindiko amesema Katika ushirika ambao unanunua mazao Mkoani hapa katavi kampuni ya GBS haijawahi kuwa na changamoto ya ulipaji hivyo ni chachu Kwa wakulima kuendelea kuzalisha Kwa wingi ili Ili kujikimu binafsi na kukuza uchumi wa mkoa.

Mkuu wa mkoa wa katavi Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindiko alipokuwa akihutubia wanacnhi wa kijiji cha Makongoro Katika hafla ya uzinduzi wa msimu wa masoko ya Pamba, tumbaku na mazao mchanganyiko. Picha na Festo Kinyogoto
Awali akitoa tathmini ya kilimo kwa mkoa wa katavi kaimu katibu tawala wa mkoa wa Katavi NEHEMIA JAMES amesema mkoa umefanikiwa kizalisha kilo milioni 12 Kwa mwaka huu huku sababu ya uazalishaji huo ukiatajwa kuwa ni uwepo wa Kiwanda kimoja kilichopo halmashari ya wilaya ya Tanganyika pamoja na maji kituama, magonjwa shambulizi na wakulima kutofuata mbinu za ugani.

Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Katavi NEHEMIA JAMES wakati akitoa tathini ya kilimo. Picha na Festo Kinyogoto
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa zao hilo wamesema uwepo wa soko Hilo unatoa hamasa ya uzalishaji kwao kwakuwa hawatapata ugumu wa kuuza mazo pale unapofikia muda wa mavuno licha ya kuwa Bei ipo chini hivyo wamewaomba wanunuzi kuongeza Bei ili waweze kunufaika zaidi.
Mrindiko ameagiza kuhakikisha malengo ambayo yanapangwa yanafikiwa Kwa wakulima kufuata mbinu za kilimo, na wataalamu kuhakikisha tathimini inafanyika ili kulinganisha na misimu mingine na kwanini imekuwa vigumu kufikia lengo la kuzaliza Tani milioni 50.

Baadhi ya wakulima na wananchi waliohudhuria hafla hiyo. Picha na festo kinyogoto